Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmed al-Qattan, rais wa Jumuiya ya «Qulna wal-‘Amal» na mwanazuoni wa Kisunni wa Lebanon, katika hotuba yake ya kisiasa ya kila wiki kutoka mji wa Brāliyās katika mkoa wa Bekaa, alibainisha kwamba; watu wote hivi karibuni wameona ni kwa kiasi gani adui wa Kizayuni ameongeza kuzunguka kwake angani na uvamizi wake wa kila siku dhidi ya maeneo na vijiji vyetu; na hili, kama lina maana yoyote, linaonesha kwamba; adui huyu hafuati maazimio, wala ahadi na makubaliano.
Aliongeza kuwa: Yeyote anayefikiri vingine, yuko katika udanganyifu; adui huyu hafuati maazimio wala mkataba.
Sheikh al-Qattan aliwataka watu wajumishe nia na kutilia maanani kinachoendelea huko Ghaza, akisema: Ni vipi watu wetu na ndugu zetu, wapiganaji mashujaa, wapo katika kukabiliana na adui huyu, hata baada ya kudai kwake kuzingatia makubaliano ya kusitisha mapigano, wakati kila siku anavunja makubaliano hayo huko Ghaza, Lebanon na mahali popote pale ambako adui huyu ameweka mguu wake? Hakika, msisite — yeye hataweza kuzingatia mikataba, ahadi na makubaliano.
Mwanazuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon alimsifu Rais wa Jamhuri na Kamanda wa Jeshi la Lebanon kwa misimamo yao ya uwajibikaji, pamoja na kila msimamo wa kitaifa unaoonesha umoja wa Walebanoni na jinsi walivyo ungana katika kukabiliana na adui huyu, akasema: Tunaheshimu na kuthamini misimamo hiyo, lakini ni masikitiko kwetu kuona baadhi ya watu wa nchi yetu na makundi yanayodai ni Walebanoni ambao kwa maneno yao, kwa bahati mbaya, kwa kila neno wanalozungumza, wanamtumikia adui.
Alibainisha kuwa: Katika wakati huu mgumu tunaoishi, tunastahili kuwa na mshikamano wa kitaifa na wa Kiislamu kuliko wakati wowote ule, na tunapaswa kuziba njia kwa adui huyu na kuuonesha ulimwenguni kwamba Lebanon ni imara na ina uwezo mkubwa wa kumzuia na kumkabili adui huyu.
Sheikh al-Qattan alisisitiza: Hatutachukua msimamo mwingine isipokuwa ule wa kupigana na adui huyu, hata ikiwa itabidi kujitolea kwa aina yoyote ile, hata kwa kupata shahada, tutakabiliana na uvamizi na mashambulio ambayo adui huyu anayafanya.
Maoni yako